Habari

Mr Blue aongelea majukumu yake kama baba, aumalizia mjengo wake, kuhamia Jan 1

Hitmaker wa Pesa, Mr Blue aka Kabayser amesema tangu awe baba, maisha yake yamebadilika na haishi kama zamani tena.

11036c86567c11e3b8d2126f3d3312b1_8
Mr Blue na mwanae Sameer

“Nafikiri kwa mimi imenikuza zaidi,” Blue ameiambia Bongo5.

Hata hivyo amesema pamoja na kuwa baba, majukumu aliyonayo hayajabadilika sana japo kwa sasa amekuwa yeye binafsi na familia yake. “Kilichobadilika kwangu ni bidii kuongezeka inabidi niangalie familia yangu iandaje.”

f33b6dfc5f6d11e3948f0a4825b4191e_8
Wahyda (mchumba wake na Blue) akiwa na mwanae Sameer

“Ni mtu kwakweli kama baba yake na mimi nafurahi,” Blue amemuongea mwanae huyo wa kiume aitwaye Sameer. “Inabidi amrithi baba yake tu kwa uchakarikaji na kila kitu.”

da9d65ca5f0411e39dc812f864d4b6c0_8
Wahyda

Katika hatua nyingine Mr Blue amesema tayari amemalizia mjengo wake na anatarajia kuhamia tarehe 1 January 2014.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents