Michezo

David Luiz: Sijui tutafanya nini ili tuwaone tena Wabrazil wakitabasamu!

Nahodha wa muda wa Brazil, David Luiz amewataka mashabiki wa timu hiyo kote duniani kuwasamehe wachezaji waliokuwa uwanjani Selecao ilipoadhibiwa kichapo cha mabao 7-1 na Ujerumani katika mechi ya kwanza ya nusu fainali ya kombe la dunia huko Brazil.

140708233422_luiz_akilia_baada_ya_kushindwa_na_ujerumani__512x288_bbc_nocredit
David Luiz akilia kwa uchungu baada ya kipigo cha goli 7-1

Luiz ambae alionekana akilia kwa machungu alisema amini usiamini Ujerumani ilikuwa inaongoza mabao 5-0 kufikia dakika 29 ya kipindi cha kwanza. “Wajerumani walikuwa timu bora zaidi yetu, ni siku ya majonzi tele kwa Wabrazil, mtuwieni radhi sijui tutafanya nini ilituwaone tena wabrazil wakitabasamu,?” Alisema Luiz

Kilio kimezidi kote nchini humo haswa baada ya nyota wa Brazil Neymar kujeruhiwa uti wa mgongo Ijumaa iliyopita katika mechi ya kufuzu kwa nusu fainali dhidi ya Colombia. Kwa Upande wake Kipa wa Brazil Julio Cesar alitaja dakika hizo kumi timu hiyo ilipofungwa mabao manne kuwa sawa na kuzimia.

Source:BBC

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents