Bibi Cheka kula sahani moja na Wana Hip Hop
Bibi Cheka si mgeni katika fani ya muziki, lakini ni mgeni katika uimbaji wa muziki hasa baada ya miaka ya sabini, kuwa miongoni mwa wanamuziki kumi na sita katika kundi la Makocha ambao walikuwa wakinengua na kusasambua kwenye bendi ya Msondo Ngoma kitambo hicho.
Zaidi na zaidi bibi huyo alikaa na kufikiria hasa baada ya kufikiria kwamba ng’ombe atazeeka lakini maini bado yatakuwa yakijana kwakuwa maini hayazeeti, pia ndipo akajipima na yeye kuona umbo limzeeka lakini sauti na uwezo bado upo na kuamua kurudi tena kwa kasi kwenye idara ya muziki wa kisasa maarufu kama Bongo Fleva, huku akiwapa ahadi kibao mashabiki wake kama atawagongea mpaka Hip Hop, RnB na ngoma za asili pia yumo, ila akasema kwenye taarabu hapo hatogusa kwakuwa hana hulka na nyimbo hizo na kubaki kama shakibi.
Hivi sasa mwanamziki huyo ameshakamilisha wimbo wake wa Ni wewe katika sttudio ya Poteza Record chini ya Producer Mr India Suresh, na hivi sasa kuanzia kesho anaanza kushoot video ya wimbo huo, ili mtakapokuwa mnamsikiliza pia mumuone kwenye kitu cha Chupa…