Habari

TMK Wanaume kupiga Konzi 1 manundu 10,000

TMKBaada ya kimya kilichotiliwa shaka na wapenzi wa burudani hapa nchini, kundi la TMK wanaume hivi karibuni linatarajiwa kuzindua albam yao ambayo inatarajiwa kuwa mitaani kuanzia tarehe 15 mwezi September.

TMK


Baada ya kimya kilichotiliwa shaka na wapenzi wa burudani hapa nchini, kundi la TMK wanaume hivi karibuni linatarajiwa kuzindua albam yao ambayo inatarajiwa kuwa mitaani kuanzia tarehe 15 mwezi September.


Bongo5 ilipata fursa ya kuongea na baadhi ya wasanii wa kundi hilo, ambapo walidai kuwa, albam imeshakamilika kinachosubiriwa ni muda wa kuitupa marikiti kwani inaaminika kuwa mashabiki wana kiu kubwa sana kusikia shughuli toka kwa watoto wa kiumeni.


“ujio wetu kila mtanzania anausubiri kwa shauku, na ukimya wetu ulisababishwa na maandalizi kwani tusingependa kuipa jamii kile ambacho hakiwastahili nikiwa na maana bidhaa famba, ukizingatia kila msanii wa TMK ni kichwa” alisema Temba ambaye kwa anatamba na jiwe lake ‘mwaka wa shetani’


Imeshazoeleka kuwa mapanga ndio staili bora kabisa nchini hasa unapolitaja kundi la TMK wanaume lakini safari hii jamaa wanakuja na staili mpya kibao “ili kuonesha kuwa sisi hatupimiki tumeamua kuja na staili mpya kabisa za uchezaji ikiwa ni pamoja na ‘tulia hivyo hivyo, konzi moja manundu elfu kumi’ na nyingine ambazo zitakuwa ni surprise kwa mashabiki.


Mpaka hivi sasa Jamaa wanatamba na ngoma zao kama ‘kazi ipo’ inayobeba jina la albam pamoja na ‘pisha njia’ ambayo iko hewani na ina Bang ile mbaya.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents