Habari

Adama Barrow amteua Fatoumata Tambajang kuwa makamu wake wa Urais Gambia

Rais mpya wa nchi ya Gambia, Adama Barrow amemteua mwanamama Fatoumata Tambajang kuwa makamu wa Rais wa nchi hiyo.

Uteuzi huo umetangazwa na msemaji wa Rais Barrow, Halifa Sallah kwenye mkutano wa waandishi wa habari uliofanyika mjini Banjul Jumatatu hii ambapo pia linatarajiwa kutangazwa baraza la mawaziri mapema wiki hii.

Tambajang aliwahi kufanya kazi katika shirika la Umoja wa Mataifa la UNDP na kushikilia madaraka ya uwaziri wa Afya na Ustawi wa Jamii katika nchi hiyo. Imedaiwa kuwa Fatoumata alikuwa akipingana vikali na Rais Yahya Jammeh ambaye ameachia madaraka siku chache zilizopita.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents