Technology

Akaunti ya Twitter ya Rais Donald Trump yapotea hewani kwa muda

Akaunti ya Rais wa Marekani, Donald Trump ya mtandao wa Twitter ilipotea kwa muda wa dakika 11 hewani na kisha kurejea tena hewani baada ya makosa kurekebishwa na mtandao huo.

Tokeo la picha la trum twitter acount deactivated

Twitter wamethibitisha kwa kueleza kuwa kulitoa tatizo la kibinadamu kwenye kampuni yao ambapo moja ya mfanyakazi wao aliisitisha kwa muda (Deactivated) akaunti ya Trump lakini baadae wakagundua tatizo hilo na kuirudisha hewani.

Twitter wameeleza kuwa mfanyakazi huyo aliifuta kimakosa kipindi akijiandaa kuondoka jana usiku lakini wataendelea na uchunguzi zaidi juu ya tukio hilo.

Kitendo hicho cha kupotea kwa muda akaunti hiyo kimewafurahisha baadhi ya watu wanaopinga misimamo na itikadi zake za kiutawala.

Hata hivyo tayari ukurasa huo wa Rais ,Donald Trump (@RealDonaldTrump) umerejea hewani na mwenyewe hajazungumzia chochote mpaka sasa hivi.

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents