Burudani

Alichosema Nedy Music kuhusu hali ya Ommy Dimpoz

Msanii wa muziki Bongo, Nedy Music amefunguka kuhusu kuuguwa kwa Ommy Dimpoz.

Muimbaji huyo ambaye anasimamiwa na label ya Ommy Dimpoz ‘PKP’ amesema kwa kipindi hiki ambacho Dimpoz anaumwa kuna vingi anavikosa kutoka kwake.

“Kuna vitu vingi ambavyo navimisi kutoka kwa Ommy Dimpoz haswa kipindi hiki anachoumwa. Ni mtu ambaye ananishauri mambo mengi, na mara nyingi huwa tunakaa na kusikiliza kazi zetu,” Nedy Music ameiambia Clouds FM.

Utakumbuka May 2018 Nendy Music alimshirikisha Ommy Dimponz katika wimbo wake uitwao Usiende Mbali. June 15, 2018 ndipo Ommy Diampoz aliweka wazi kwa mashabiki wake kuwa yupo nchini Afrika Kusini kwa ajili ya matibabu ambapo alifanyiwa upasuaji wa koo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents