Burudani

Alikiba, Marioo na Harmonize kukiwasha Jukwaa moja Leo

Wasanii nguli wa Mziki wa Bongo Fleva hapa nchini Alikiba, Marioo na Harmonize wametajwa kuwa miongoni mwa wasanii 10 wakubwa ambao watauwasha moto wilayani Muheza wakati wa Mkesha wa Mbio za Mwenge wa Uhuru leo April 15, 2024.

Mkesha duo wa mwenge wa Uhuru utakuwa chini ya Udhamini wa Rais wa Crown Media Alikiba na utafanyika kwenye Uwanja wa Jitegemee Wilayani Muheza huku wananchi mbalimbali wakukaribishwa kushiriki.

Akizungumza na waandishi wa Habari kenye eneo la Kivutio cha Utalii cha Magila Wilayani Muheza Mkuu wa Wilaya ya Muheza Zainabu Abdallah alisema kwamba maandalizi ya mbio hizo yamekamilika na wasanii hao wamekwisha kuingia wilayani humo kwa ajili ya kutoa burudani kwa wazazi wa mji huo.

“Maandalizi ya Mwenge wa Mapokezi ya Mwenge wa Uhuru yanaendelea vizuri na tunategemea tutaupokea katika Kijiji cha Mkanyageni na utakimbizwa katika miradi mbalimbali iliyopangwa hivyo nitoe wito kwa wananchi kujitokeza kuulaki kila utakapokuwa umepita Alisema.

Katika Jukwaa hilo la mkesha wa Mwenge Mbunge wa Jimbo la Muheza (CCM) Hamisi Mwinjuma ambaye pia ni Naibu Waziri wa Michezo, Sanaa na Utamaduni atakuwa sehemu ya wasanii ambao wanatumbuiza kwenye tamasha hilo.

Wasanii wengine ambao watalipamba jukwaa hilo licha ya hao ni Bilnass, Ommy Dimpoz, Maua Sama, Dulla Makabila, Chino, Kontawa ambar watatoa burudan kwa wakazi wa mji wa Muheza katika mkesha wa Mwenge wa Uhuru utakaofanyika kwenye wilaya ya Jitegemee.

Akizungumza Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo hilo MwanaFA alisema mkesha wa mwenge wa Uhuru mwaka huu utakuwa Babu kubwa na utafunika maeneo mengine ambazo utakuwa umekesha kutokana na maandalizi waliyoyafanya.

“Lakini kubwa tunajivunia aina ya miradi ni mizuri na mikubwa nitre shukrani kwa Rais Samia Suluhu kwa kutuwezesha kawa na miradj hiyo kazi yetu ni kuendelea kuomba na uwepo usimamizi wa Fedha zinazokuja Muheza haziwezi kuingia shimoni bali zinatumika kutatua changamoto za Wananchi“ Alisema

Hata hivyo kwa upande wake msanii Maua Sama ambaye ameteuliwa kuwa Balozi wa Mazingira alishukuru kwa kupata nafasi ya kuwa balozi pamoja na yote, vijana wana mambo mengi wanakwenda kufanya pamoja na watashirikiana.

Hata hivyo kwa  upande wake msanii Mwijaku alimpongeza Rais Dkt Samia Suluhu kwa namna anavyosimamia ilani ya CCM na maono ya Rais Samia Kiongozi wa kweli ambaye hupigania uwekezaji wa maendeleo na wanahitaji maendeleo ya kweli na sio Viongozi wenye maneno maneno.

Mwijaku pia alimpongeza Rais Dkt Samia Suluhu na Mkuu wa wilaya ya Muheza Zainabu Abdallah kwa kuendelea kuifungua Nchi kwa miradi mbalimbali ya kimkakati ya maendeleo.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Chanzo: Tanzaniaweb.Live

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Imeandikwa na Mbanga B.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents