Habari

Aliyekuwa mlinzi wa rais wa Rwanda Kagame, ahukumiwa kifungo cha maisha jela – Video

Aliyekuwa mlinzi wa rais wa Rwanda ahukumiwa kifungo cha maisha jela - Video

Mahakama ya rufaa mjini Kigali imethibitisha hukumu ya kifungo cha maisha jela dhidi ya Luteni Joel Mutabazi ambaye alikuwa mlinzi wa karibu wa Rais wa Rwanda Paul Kagame.

Hatua hii imechukuliwa baada ya bwana Mutabazi kukata rufaa kupinga hukumu hiyo aliyopewa mwaka 2014 baada ya kupatikana na hatia ya kutaka kuangusha serikali na kutaka kumuua Rais Kagame.

Yve anasema kuwa kesi hiyo ilichukua muda mrefu kutokana na kwamba idadi ya wahusika walikuwa kwa jumla walikuwa watu 9 akiwemo Luteni Joel Mutabazi ambaye yeye mwenyewe alishtakiwa makosa 8.

Baada ya mahakama ya rufaa kuyachambua mashtaka hayo jinsi yalivyo kulingana na faili la mashtaka la kila mtu, imeamua kutoa hukumu ya kifungo cha maisha jela kama ilivyotolewa mahakama kuu ya kijeshi dhidi ya Joel Mutabazi mwaka 2014.

Mahakama imesema kwamba kuna ushahidi wa kutosha wa kuhusika kwake kwa makosa makubwa ya kuhatarisha usalama wa taifa.

Kwa kuwa bwana Mutabazi alikuwa akitakaa kuiangusha serikali na alifanya ugaidi kwa kushirikiana na makundi ya waasi ambayo ni pamoja na RNC (Rwanda National Congres) linaloiongozwa na mkuu wa zamani wa majeshi ya Rwanda Jenerali Kayumba Nyamwasa na kundi la FDLR.

Lakini kikubwa zaidi ni kutaka kumuua rais Paul Kagame ili kufuta ushahidi kwamba ,Luteni Joel Mutabazi alisuka njama ya kulipua boti la Rais katika ziwa Muhazi karibu na makazi ya Rais Kagame.

Rwanda

Joel Mutabazi alikuwa mlinzi wa karibu sana wa rais Kagame akihusika na makazi ya rais yaliyoko katika ziwa Muhazi mashariki mwa Rwanda.

Yeye hoja zake za kukata rufaa zilikuwa kwamba alizuiliwa kinyume na sheria, akisisitiza kwamba alitekwa nyara alipokuwa uhamishoni nchini Uganda.

Vilevile alihoji kuwa wakati anakamatwa hakuwa tena askari wa Rwanda je kuna haja gani kwa kesi yake iliendeshwa na mahakama kuu ya kijeshi.

Askari wengine 8 walioshtakiwa pamoja pia hukumu dhidi yao za vifungo kati ya miaka 10 na 25 zimedumishwa isipokuwa mmoja tu Kalisa Innocent aliyepunguziwa adhabu na kupewa kifungo cha miaka 12 jela badala ya 25.

Mnamo Januari mwaka 2014, watu 16 nchini Rwanda walifikishwa mahakamani kwa tuhuma za kupanga njama ya ugaidi.

Washitakiwa hao ni pamoja na aliyekuwa mlinzi wa Rais Paul Kagame (Joel Mutabazi).

Mashirika ya kutetea haki za binadamu yamekuwa yakielezea wasiwasi kuhusu tisho dhidi ya maisha ya wapinzani wa serikali ya Kagame.

Awali afisa mmoja mkuu katika Umoja wa mataifa, amekosoa namna ambavyo serikali ya Rwanda inawatendea wanasiasa wa upinzani.

Ikiwa baadhi yao walikamatwa na kufungwa jela kwa kile kilichosemekana kuwa kueneza uvumi.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents