Habari

Amjeruhi baba mkwe kwa risasi nje ya kanisa

Mtu mmoja amejeruhiwa kwa risasi pembeni ya kanisa wakati akitaka kuingia katika Kanisa Katoliki, Parokia ya Kibangu, wilayani Ubungo jijini Dar es salaam ambapo una daiwa ni ugomvi wa kifamilia.

Tukio hilo limetokea Jumapili hii na aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Suzan Kaganda alithibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo amesema mtuhumiwa anashikiliwa na jeshi la polisi ambapo majeruhi amelazwa katika hospitali ya Muhimbili.

“Tumebaini kwamba yule mwanananchi aliyemshambulia mhusika ni ambaye ni victim ni mtu na baba mkwe wake, kwahiyo ni mambo ya kifamilia zaidi tuko nae tuna muhoji tuweze kujua kulikoni na hatimae tuweze kuchukua hatua za kisheria,” alisema.

“Lakini katika mahojiano tu ya awali tunaona kulikuwa na mgongano wa kimaamuzi katika familia kwasababu ukiangalia ni baba mkwe au tuseme ameoa mtoto wa huyu mzee aliyejeruhiwa na majeruhi tumempeleka pale Muhimbili kwaajili ya tiba wakati tuna muacha Muhimbilia alikuwa amepigwa kwenye bega na hali yake ilikuwa inaendelea vizuri hatukuweza kusema sana mambo ya kitabibu tunawaachia wenzetu.”

Na Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents