BurudaniUncategorized

Ariana Grande na mastaa hawa ndani ya show nyingine Manchester

Baada ya show ya ziara ya Ariana Grande “Dangerous Woman World Tour” ya mjiji Manchester kuingia dosari kutokana na mlipuko uliosababisha vifo vya watu 22 na majeruhi zaidi ya 50 wiki iliyopita, muimbaji huyo amewataja wasanii wengine atakaoungana nao katika show nyingine mji humo Juni 5.

Ijumaa iliyopita msanii huyo wa muziki wa Pop aliweka barua katika mtandao wake wa kijamii akiahidi kurudia kufanya show nyingine mjini Manchester kwa ajili ya kufurahi pamoja na mashabiki wake kwa kuwafuta machozi kutokana na tukio hilo la kusikitisha.

Kwa mujibu wa mtandao wa Billboard, Ariana ametaja jina la show hiyo kuwa ni “One Love Manchester” ambapo atatarajiwa kutumbuiza na wasanii wengine akiwemo Justin Bieber, Coldplay, Katy Perry, Miley Cyrus, Pharrell, Usher, na Niall Horan.

Show hiyo itafanyika katika uwanja wa Emirates Old Trafford Cricket Ground ambao unauwezo wa kuchukua watu 50,000 na tiketi zake zinatarajiwa kuanza kuuzwa leo (Jumanne). Lakini pia show hiyo inatarajiwa kuruka moja kwa moja kupitia BBC TV, BBC Radio na Capital Radio Networks.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents