MichezoUncategorized

Australian Open 2018: Cilic atinga fainali kumsubiri mbabe wa Nadal au Roger Federer

Mcheza tenisi kutoka nchini Croatia, Marin Cilic amefanikiwa kutinga katika hatua ya fainali baada ya kumchapa mpinzani wake Kyle Edmund katika hatua ya nusu fainali.

Cilic amefanikiwa kutinga katika hatua hiyo kwa ushindi wa seti 6-2 7-6 (7-4) 6-2.

Kutokana na ushindi huo, Cilic anaweza kupanda mpaka nafasi ya tatu katika viwango vya ubora wa mchezo huo duniani vitakavyotoka wiki ijayo.

Kwa sasa mchezaji huyo ana subiri kucheza fainali na mshindi wa mchezo kati ya Roger Federer na Hyeon Chung ambao watachuana kesho (Ijumaa).

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents