BurudaniVideos

Azma aeleza alivyompata Sugu kwenye ngoma yake mpya ‘Garagasha’ (Video)

Kwa status ambayo Sugu anayo – mbunge wa Mbeya Mjini, si rahisi kwa msanii kumpata na kumshirikisha kwenye ngoma yake.

Na ndio maana Azma amepokea sifa nyingi baada ya kumshirikisha rapper huyo mkongwe kwenye wimbo wake Garagasha. Akiongea na Bongo5, Azma amesema Sugu hakuwa amemfikiria kumshirikisha mwanzoni.

Amesema wimbo huo alikuwa amepanga kuwashirikisha One The Incredible na Nikki Mbishi ambao walionesha kutingwa na mambo mengi. Baadaye Ezden na rapper wa Kenya Noti Flow waliingiza verse zao lakini Azma akaona zimepwaya.

Mwingine aliyeweka sauti yake ni Wakazi ambaye baada ya Azma kupata wazo la kuwashirikisha Izzo na Sugu verse yake ilitolewa ili aje kuitumia kwenye remix.

Amesema Sugu hakuwa mgumu kukubali kushiriki kwenye wimbo huo kutokana na Azma na Izzo kutokea Mbeya. Na hata kwenye kufanya video, Azma anasema Sugu alikuwa na ushirikiano wa kutosha na ndiye alikuwa wa kwanza kufika location.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents