Michezo

Baada ya kushindwa EPL: Claudio Ranieri atimkia Ufaransa

Meneja wa zamani wa Klabu ya Leicester City,  Claudio Ranieri amepata shavu la kuinoa klabu ya Nantes ya nchini Ufaransa.

Tokeo la picha la Claudio Ranieri nantes
Claudio Ranieri

Klabu hiyo inayoshiriki ligi kuu nchini Ufaransa (Ligue 1) walipewa ruhusa maalum na wasimamizi wa Ligi Kuu ya Ufaransa kumsajili Muitaliano huyo, ikizingatiwa kwamba alitimiza umri wa juu zaidi unaoruhusiwa kwa waamuzi, ambao ni miaka 65.

Ranieri aliiongoza Klabu ya Leicester City kunyakua taji la ubingwa wa EPL msimu wa 2015 -16 na kuongeza umaarufu kwa klabu hiyo, Kabla ya kutimuliwa mwezi februari mwaka huu baada ya kupoteza mechi tano mfululizo za Ligi kuu England.

Ranieri anachukua nafasi ya Sergio Conceicao winga wa zamani wa kushoto wa Ureno baada ya kuondoka klabuni hapo akielekea Porto.

Ranieri ana uzoefu wa kufanya kazi nchini ufaransa, kwani aliiwezesha klabu ya Monaco kupanda daraja kujiunga na Ligue 1 mwaka 2012 -13 na kuwaongoza kumaliza katika nafasi ya pili nyuma ya Paris St Germain msimu uliofuata kabla ya kuiaga timu hiyo.

Nantes itakuwa timu ya 17 kwa Ranieri kama meneja kwa miaka 31 na ambapo amekuwa mkufunzi pia wa klabu kubwa zaidi za Italia isipokuwa AC Milan.

Atletico Madrid, Chelsea na Valencia ni baadhi ya klabu nyingine ambazo ameshawahi kuziongoza kama meneja.

Klabu ya Nantes ambayo imeshinda taji la Ufaransa mara nane halijawahi kushinda taji hilo tangia mwaka 2001.

By Godfrey Mgallah

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents