Michezo

Barcelona: Kwaheri Luis Enrique hakika umefanya makubwa

Klabu ya soka ya Barcelona ya nchini Hispania imemteua Ernesto Valverde, kuwa kocha mkuu na kupokea kijiti kilichoachwa na Luis Enrique, ambaye ameiongoza klabu hiyo kwa mafanikio makubwa ndani ya utawala wake.

Aliekuwa kocha wa Barcelona, Luis Enrique

Valverde, ameingia mkataba wa miaka miwili, ambapo anaweza akaongezewa mwaka mwingine wa tatu kulingana na mafanikio mazuri atakayo yaonyesha klabuni hapo. Kocha huyu aliwahi kuwa miongoni mwa wachezaji wazamani wa kikosi hiko cha Barca, alipokuwa akicheza nafasi ya ushambuliaji.

Aliekuwa kocha wa Barcelona, Luis Enrique akimshauri kitu mchezaji Lionel Mess

Kabla ya kutua Barca, Valverde, alikuwa akikihudumia kikosi cha Athletic Bilbao kwa muda wa miaka minne.

Enrique, kabla ya kukiachia kijiti cha kuinoa Barca, amekiongoza kikosi hiko kushinda mataji matatu makubwa katika  msimu wake wa kwanza,  mataji mawili ya nyumbani mwaka 2016 na Kombe la Mfalme au Copa del Rey mwaka huu.

Kocha wa sasa wa Barcelona, Ernesto Valverde

Katika mchezo wake wa mwisho akiwa kama kocha alishinda jumla ya magoli 3 kwa 1 dhidi ya klabu ya Alaves ikiwa ni fainali ya Kombe la Mfalme .

Rais wa Barca,  Josep Maria Bartomeu alimsifu Valverde, 53, kwa uwezo wake, ufahamu, ujuzi na busara na kusema: “Huwa anaendeleza wachezaji chipukizi na hucheza mtindo wa Barca.”

BY HAMZA FUMO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents