Michezo

Karibuni kwenye mikiki mikiki ya EPL – Huddersfield Town

Klabu ya soka ya Huddersfield Town, imepanda daraja kucheza Ligi kuu nchini Uingereza EPL kwa mara ya kwanza baada ya kuilaza klabu ya Reading kwa jumla ya magoli 4-3 ushindi uliopatikana kwa njia ya mikwaju ya penati mchezo uliochezwa katika uwanja wa Wembley hapo jana.

Baada ya kutoka sare tasa ya bila kufungana ndani ya dakika 120, katika hatua ya nusu fainali Town walifanikiwa kuwaeunga wapinzani wao klabu ya Sheffield kwa mikwaju ya penati.

Christopher Schindler aliwashindia Town baada ya mkwaju wa Liam Moore kupaa angani , nao mpira wa Jordan Obita ukaokolewa na kipa Danny Ward.
Klabu hiyo ya Yorkshire Magharibi haija tinga katika ligi kuu nchini Uingereza tangu kuanzishwa kwake mwaka 1972.

Reading, waliomaliza kwa alama nne na kushika nafasi ya pili juu ya Town, waliokuwa nafasi ya tano katika msimamo wa ligi, wametolewa katika hatua ya mtoano wa kufuzu kupanda daraja na kushiriki ligi kuu EPL.

BY HAMZA FUMO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents