Burudani

Barua Pepe za Sony zilizovuja zabainisha mkuu wa kampuni hiyo anataka Idris Elba awe James Bond mpya!

Barua Pepe za kampuni ya Sony zilizovujishwa na hackers wanaohusishwa na Korea Kaskazini, zimeonesha kuwa mwenyekiti mwenza wa Sony Pictures Entertainment, Amy Pascal kumpendekeza Idris Elba kuwa muigizaji ajaye wa filamu za James Bond.

1419028134997.cached

Tangu zianze, mhusika mkuu wa filamu hizo ajulikanaye pia kama 007 amekuwa ni mzungu.

Kwenye email iliyotumwa January 4, 2014, kutoka kwa Pascal kwenda kwa Elizabeth Cantillon, aliyekuwa makamu mkuu wa rais wa Columbia Pictures inayosambaza filamu za Bond, aliandika kwa ufupi: Idris should be the next bond.”

Hackers hao wanadaiwa kuvujisha pia script ya filamu mpya ya James Bond, Spectre, inayotarajiwa kuingia sokoni November 6, 2015. Bajeti ya filamu hiyo ni dola milioni 300.

Kwa miaka mingi, kumekuwepo na mapendekezo mengi kuwa Idris Elba, anatakiwa kuwa James Bond ajaye na hivyo kumfanya awe 007 mweusi wa kwanza.

Chanzo: The DailyBeast.com

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents