Habari

Biden aunga mkono maandamano Cuba

Rais wa Marekani Joe Biden ameunga mkono maandamano ya Cuba na kuwasifu maelfu ya raia wa nchi hiyo walioandama kupinga uhaba wa chakula na bei za juu za bidhaa katika wakati huu wa janga la virusi vya corona.

Maandamano hayo ya kuipinga serikali ya Cuba yanatajwa kuwa ni makubwa kuwahi kushuhudiwa katika miaka ya hivi karibuni. “Marekani inasimama pamoja na watu wa Cuba wanaopigania haki zao za msingi na tunaitolea wito serikali ya Cuba kujizuia kutumia nguvu dhidi yao au kuinyamazisha sauti ya watu wa Cuba,” amesema Biden.

Tamko hilo la Biden limeonyesha msimamo tofauti na wa mtangulizi wake wa chama cha Democratic Barack Obama, ambaye wakati wa uongozi wake alijaribu kupunguza mivutano kati ya Marekani na Cuba pamoja na kuilegezea nchi hiyo vikwazo ilivyokuwa imewekewa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents