Burudani

Bill Nass azidi kuitolea macho kolabo na Alikiba

Rapper Bill Nass ameeleza bado nia yake ya kufanya kolabo na msanii Alikiba ipo pale pale.

Bill Nass ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma ‘Mazoea’ ameiambia The Playlist ya Times Fm uwezo wa Alikiba kubadilika kwenye kila kolabo ndio unamshawishi kufanya hivyo.

“Ikiwezekana kwa sababu ni mmoja kati ya watu ambao nawaona, kolabo ambazo amewahi kufanya mapokezi yake (makubwa), yuko flexible kwenye collaboration anafaa” amesema Bill Nass.

“Alikiba ni moja kati ya wasanii ambao wamebisha kwa sababu ana muda mrefu kwenye game nimekuwa nikimsikia nikiwa bado hata sijafikiria kufanya muziki lakini bado anafanya vizuri, ngoma kama Seduce Me nimeiona mbali sana nimependa production yake” ameongeza.

Mwana FA, Godzilla na Mr. Blue ni miongoni mwa wasanii wanaofanya muziki wa rap ambao waliweza kumshirikisha Alikiba katika ngoma zao na aliweza kuzitendea haki chorus za ngoma hizo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents