Habari

Rais Trump atangaza tarehe na mahali atakapokutana na hasimu wake Kim Jon-Un

Rais wa Marekani, Donald Trump ametangaza tarehe na mahali ambapo atakutana na kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jon-Un.

Tokeo la picha la trump
Donald Trump

Rais Trump ametangaza kupitia ukurasa wake wa Twitter, amesema atakutana na Kim Jong-un nchini Singapore mnamo tarehe 12 Juni mwaka huu.

Trump mwezi Aprili mwaka huu alitangaza kuwa atakutana na kiongozi huyo jambo ambalo watu wengi hawakuamini kutokana na marumbano ya marais hao kwa muda mrefu.

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents