Habari

Serikali yajenga viwanda vipya 3,306

Serikali ya Awamu ya Tano tangu iingie madarakani imefanikisha Ujenzi wa Viwanda zaidi ya 3,306 vikubwa na Vidogo hadi kufikia machi 2018.

Akiwasilisha Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi, Waziri wa Viwanda Biashara na uwekezaji, Charles Mwijage amesema kuwa ujenzi wa viwanda hivyo unatokana na dhamira ya Serikali kujenga uchumi wa viwanda ili kukuza ajira na uchumi.

“Kwa mujibu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, hadi kufikia mwezi Machi 2018, nchi yetu ilikuwa na jumla ya viwanda 53,876. Kati ya hivyo, viwanda vikubwa ni 251 vya kati ni173, vidogo ni 6,957 na vidogo sana ni 46,495. Kwa kipindi ambacho Serikali ya Awamu ya Tano imeingia madarakani, chini ya uongozi mahiri wa Rais wetu Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, hadi Machi
2018, viwanda vipya 3,306 vimejengwa’’ Alisema Mwijage.

Akifafanua Mwijage amesema kutokana na dhamira safi ya Serikali kujenga uchumi wa Viwanda hali iliyopelekea Tanzania kujitosheleza kwa mahitaji ya nondo, mabati, vinjwaji na vigae.

Katika kufufua viwanda vilivyosimama kuzalisha, Mwijage amesema kuwa msimamo wa Serikali nikuhakikisha kiwanda cha matairi Arusha kinafanya kazi na jukumu la kuboresha na kuendesha kiwanda hicho litakuwa mikononi mwa sekta Binafsi huku Serikali ikibaki na hisa kulingana na rasilimali zilizopo.

Akizungumzia vipaumbele vya Wizara kwa mwaka 2018/19, Mwijage amesema kuwa ni kuendeleza miradi ya kielelezo ya Mchuchuma na Liganga, Magadi soda Engaruka na Kiwanda cha Matairi Arusha, Uendelezaji wa eneo la Viwanda TAMCO Kibaha na mradi wa kuunganisha matrekta.

Vipaumbele Vingine ni uendelezaji wa Mitaa, Maeneo ya Viwanda vya SIDO, Kuendeleza Kanda Kuu za Kiuchumi, Ruvuma, Tanga, Kigoma, Manyoni, Bagamoyo, SZE na BMSEZ, Kurasini Logistic Centre na Kigamboni Industrial Parks.

Aidha ameongeza kuwa, kati ya Julai 2017 hadi Machi 2018 jumla ya miradi 243 yenye thamani ya dola za kimarekani milioni 3,667 imeajiri watu 36,025 na imesajiliwa na TIC, BRELA na EPZA.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents