BurudaniHabari

Chameleon anatafutwa na Polisi

ChameleoneMsanii maarufu barani Afrika Josee Chameleon anatafutwa na Police baada ya kutoweka ukumbini bila kufanya onesho kama ilivyokusudiwa na mashabiki

ChameleoneMsanii maarufu barani Afrika Josee Chameleon anatafutwa na Police baada ya kutoweka ukumbini bila kufanya onesho kama ilivyokusudiwa na mashabiki na waandaaji wa tamasha la EastAfrican ShowDown iliyofanyika kwenye ukumbi wa Mamba Club jijini Mombasa akiwa ameshalipwa mkwanja kwa ajili ya onesho hilo .

 

Kibweka cha staa huyo kilifanyika siku ya mkesha wa mwaka mpya 2006-2007 ambapo mchizi alifika mpaka ukumbini na kuaga anaenda kuchukua fegi wakati show imeshaanza na msanii Noorah akiwa jukwaani akikamua lakini alitoweka katika mazingira ya kutatanisha.

 

Waandaaji wa tamasha hilo walipostuka kuwa mchizi hayupo ikabidi watie timu hadi hotelini alipofikia wakakuta hayupo isipokuwa mabegi yalikuwepo, walipoyakagua wakakuta hakuna chochote zaidi ya makaratasi.

 

Source: Bongo5

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents