Burudani

Christian Bella hana mpango wa kutoa album

Nyota wa muziki wa dansi nchini Tanzania, Christian Bella amesema hana mpango wa kuachia album kutokana na anguko la soko pamoja na kudai kazi zake zinaishi kwa muda mrefu.

11850238_1009422202431264_216586376_n

Bella ambaye ameachia wimbo mpya pamoja na bendi yake uitwao, Amerudi, amesema amejipanga kuboresha zaidi kazi zake ili ziwe na mvuto na ziishi kwa muda mrefu kama zilizopita.

“Sina mpango wa kutoa album, sina haraka kabisa ya kutoa album,” amesema.

“Mimi natoa wimbo mmoja unakaa miaka mitatu, pia soko linazingua. Mimi nikitoa nyimbo yangu inakaa miaka mitatu nafanya show na bado inafanya vizuri, sio lazima kutoa album. Nakuhitaji ile ndio style yangu. Toka nimeitoa 2013 mpaka leo niliipiga kwenye show balaa. Ukitoa album utatoa nyimbo nyingi watu watashindwa kujua ipi ni kali ya kuisikiliza.”

“Watu hawana muda wa kukaa kuanza kusikiliza nyimbo moja moja kwenye album mpaka wajue ipi ni kali zaidi ya nyenzake. Mimi sina haraka, natoa ngoma baada ya ngoma. Ukiangalia Nashindwa ipo kwenye nafasi nzuri sana kwenye chart mbalimbali. Uzuri mmoja ngoma zangu kwenye uchochoro huko zinapigwa sana hali ambayo najipanga kwa mwaka kila baada ya miezi 2/3 natoa ngoma mpya,” aliongeza.

Kwa upande wa wimbo mpya wa bendi yake, Bella amesema Amerudi ni jibu la wimbo wa awali wa Malaika Band, Ameondoka.

“Kwanza wimbo wangu mpya Amerudi, hili ni jibu la wimbo Ameondoka, sasa yule demu amerudi. Sasa namuuliza karudi kafuata nini sasa?, Lakini hii ni kazi ya bendi yangu,” amesisitiza.

“Bendi yangu ni tofauti na bendi zote. Ukiangalia video ya Amerudi ni video nzuri, muziki ninaofanya ndani ya bendi ni muziki wa kisasa. Kila mtu ataupenda, uwe mpenda hip hop, mpenda Bongo Flava, Taarab utapenda nyimbo zake tu. Na mimi kama unavyojua siwezi kuwa msanii wa CD, mimi lazima niwe msanii wa live band, ndio maana nawakaribisha mashabiki wa muziki wa bendi pale Mango Garden Jumamosi hii waone kazi. Kutakuwa na vitu tofauti, uzinduzi wa ngoma mpya.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents