Michezo

Daniel James awaomba radhi mashabiki wa Manchester United kwa kipigo cha Burnley 

Daniel James amewaomba radhi mashabiki wa Manchester United baada ya kupokea kipigo dhidi ya timu ya Burnley hapo juzi siku ya Jumatano.

Winga huyo wa United, amesema kuwa pafomansi ya timu yao haikuwa nzuri na kuahidi kufanya vizuri katika michezo ijayo.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 ameiyambia MUTV kuwa  ”Tunajutia kwa hili, tunafahamu hatukuwa bora vya kutosha.”

”Kama timu, tunahitaji kuwa katika nafasi nzuri, tulilenga langoni mashuti mengi, pengine tulipaswa kufunga bao kutokana na nafasi tulizotengeneza.”

”Tuliamini licha ya kuwa nyuma kwa mabao 2 – 0 lakini bado tungeweza kushinda mchezo, ilitokea kwa Sheffield United, tuliamini hivyo lakini haikuwa.”

United ilipoteza mchezo huo wakiwa nyumbani katika uwanja wa Old Trafford kwa jumla ya mabao 2 – 0 dhidi ya Burnley, magoli yakifungwa dakika ya 39 na 56 kupitia Chris Wood na Jay Rodriguez.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents