Habari

Dar Mpya ya Makonda: Makonda aagiza kukamatwa kwa mwenyekiti wa Mtaa Gongolamboto

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda ameliagiza jeshi la polisi kumkamata mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Gongolamboto, Bakari Shingo baada ya kutuhumiwa kukusanya mapato kwa kutumia risiti anazozichapisha mwenyewe kinyume na Halmashauri inavyoagiza pamoja na kutoitisha mikutano ya hadhara kwa muda mrefu na kushirikina na wahalifu.

if
if
Polisi wakiwa wamemkamata mwenyekiti wa serikali ya Mtaa Gongolamboto, Bakari Shingo kwa tuhuma za kughushi stakabadhi za mapato ya mtaa huo wakati wa mkutano wa hadhara Pugu Kajiungeni Dar es salaam.

Hatua hiyo imekuja baada ya wananchi kulalamika kwa kumtuhumu mwenyekiti huyo kukaa muda mrefu bila kusoma mapato ya mtaa huo pamoja na kughushi stakabadhii za mapato.

Lawama hizo zimempelekea Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda ambaye yupo kwenye ziara yake katika wilaya ya Ilala Pugu Kajiungeni, kumuagiza Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Ilala, Salum Hamduni kumsweka rumande Mweyekiti huyo mpaka upelelezi utakapo kamilika.

Akitoa ushahidi kuhusu sakata hilo Mkazi wa Gongo la Mboto na Mjumbe wa Serikali ya Mtaa Pili Seif ameeleza kuwa hiyo imekuwa ni tabia ya mwenyekiti huyo kwa muda mrefu na taarifa zimefikishwa kwenye mamlaka husika ikiwemo kwa Mkuu wa Wilaya Sophia Mjema, Mkurugenzi Msongela Nitu na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents