Burudani

Daz Baba: Msiamini yaliyoandikwa, mimi nipo fit

Daz Baba amedai kuwa yupo gado kama Zay B tofauti na magazeti ya udaku yalivyoandika miezi ya hivi karibuni. Baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu, msanii huyo amesema anajiandaa kuja na album yake mpya.

Daz Baba akiwa kwenye mazishi

Daz Baba ameiambia Bongo5, kuachia kwake album kutawafanya mashabiki wake wapate kazi zake kwa wingi tofauti na kuachia single moja moja.

“Unajua watu wameshazusha mengi kuhusu maisha yangu lakini ninachosema kwa mashabiki wangu mimi nipo njema na harakati za muziki zinaendelea kama kawaida,” alisema.

“Nipo kwenye mchakato wa kuachia album yangu mpya ambayo nitauza mimi mwenyewe bila kutegemea mhindi. Unajua hii ni biashara kama biashara nyingine inategemea unajipanga vipi ili ufanye biashara.”

Daz Baba

Pia Daz amewataka mashabiki wake kusikiliza wimbo wake mpya uitwao ‘Pointer’ pamoja na kukaa tayari kwa ujio wa video mpya na kazi mpya akiwa na Juma Nature.

Related Articles

Leave a Reply

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents