Michezo

Dembele afungiwa mechi sita na FA

Kiungo wa klabu wa Tottenham Hotspur Mousa Dembele amefungiwa mechi sita na Shirikisho la Soka la Uingereza FA.
Ameadhibiwa baada ya kupatikana na kosa la kumshambulia mchezaji wa Chelsea Diego Costa.

33C0676D00000578-3577045-image-a-152_1462539425975

Dembele, ambaye ni raia wa timu ya taifa ya Ubelgiji, alionekana kumfinya macho mshambuliaji huyo wa Chelsea wakati wa mechi ambayo iliisha kwa sare ya 2-2.

Mwamuzi Mark Clattenburg hakumuadhibu mchezaji huyo wa mwenye miaka 28 wakati wa mechi hiyo.
Dembele aliamua kutopinga shtaka hilo na sasa hataweza kuchezea klabu yake, ambaye mkufunzi wake ni Mauricio Pochettino, hadi mechi ya tano msimu ujao.

Amechezea Spurs mechi 29 ligini msimu huu na kuwafungia mabao matatu.
Dembele alikuwa miongoni mwa wachezaji tisa wa Spurs waliooneshwa kadi ya manjano wakati wa mechi hiyo iliyochezewa Stamford Bridge.

Hiyo ni rekodi kwa wachezaji wengi zaidi kuadhibiwa kwenye mechi moja Ligi ya Premia.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents