Habari

Diamond Platnumz aingia mkataba na MTN Nigeria kuuza ‘Number 1 Remix’ kama muito wa simu

Diamond Platnumz ambaye ameondoka usiku wa kuamkia jana kuelekea Nigeria amesema kuwa baada ya Number 1 Remix aliyomshirikisha Davido kutoka, alipokea maombi mengi kutoka kwa makampuni mbalimbali ya simu ya Nigeria wakitaka kumpa dili ya mkataba wa kuuza wimbo huo kama muito wa simu (RBT/Callertune).

Platnumz na Tale
Diamond na Tale jana walipokuwa safarini wakielekea Nigeria

“Kama wiki ya tatu nilivyotoa tu nikaanza kupokea mikataba tofauti tofauti kutoka Nigeria kuwa kwenye callertune, Ringtone na kadhalika so nikasaini nao vizuri” Alisema PLatnumz.

Akiongea na Millard Ayo kupitia Top 20 ya Clouds Fm, Diamond amesema aliamua kusaini na kampuni ya simu ya MTN na kuwapa Exclusive ili apate pesa nyingi zaidi.

“So Inshallah pia naweza nikarudi na visenti vyangu ambavyo nilisaini…nilisaini na MTN peke yake kwasababu nilitaka kuwapa exclusive ili nipate pesa zaidi”.

‘Number 1’ (original) pia ilimpa dili nono Diamond hapa nyumbani ya kusaini Exclusive na Vodacom Tanzania ili kuuza kama muito wa simu Tanzania mara baada ya kutoka mwaka jana.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents