Burudani
Ex wa Big Sean aolewa na mwanaume mwingine tarehe ile ile aliyokuwa amepanga kufunga ndoa na rapper huyo
Baada ya kupigwa chini na rapper wa Good Music, Big Sean, miezi mitatu tu iliyopita, muigizaji wa TV, Naya Rivera amefunga ndoa kwa siri na mwanaume mwingine aitwaye, Ryan Dorsey.
Kama hiyo haitoshi, Naya amefunga ndoa na Ryan huko Cabo San Lucas, Mexico, Jumamosi, July 19, tarehe ambayo alikuwa amepanga kufunga ndoa na Big Sean kabla hawajaachana.
Sean na Naya waliachana na kuahirisha kufunga ndoa japo muigizaji huyo wa tamthilia ya Glee alibakia na tarehe hiyo hiyo kutimiza ndoto zake za kuolewa.