Michezo
Federer atwaa taji la BNP kwa kumchapa Wawrinka
Mcheza Tenesi Roger Federer ameshinda taji la wazi la BNP Paribas baada ya kumchapa Stan Wawrinka kwa 6-4 na 7-5.
Wawrinka anayeshika nafasi ya tatu kwa ubora alianza kwa kuongoza kwa 2-0 kabla ya Federer kurudisha na kumfunga mfululizo mpinzani wake huyo.
Stan Wawrinka
Mchezo huu ulikuwa ni wa 23 kwa nyota hawa wa tenesi kuchuana.
Elena Vesnina nae ametwaa taji la michuano hiyo kwa upande wa wanawake kwa mkumshinda Svetlana Kuznetsova 6-7 (6-8) 7-5 6-4.