AfyaHabari

Fedha ziongezwe mapambano dhidi ya Malaria- WHO

Shirika la Afya Duniani WHO leo limetoa wito wa msaada zaidi wa kifedha kusaidia kukabiliana na changamoto zinazozidi katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa malaria.

Ugonjwa huo unazidi kuwauwa mamia kwa maelfu ya watoto hasa barani Afrika kila mwaka.

Katika ripoti mpya, WHO limesema kwamba visa vya maambukizi na vifo vinavyotokana na malaria ambavyo vilikuwa vingi mwaka 2020 wakati ambapo janga la Covid-19 lililemaza juhudi za kinga na matibabu, vilisalia kwa kiwango cha kushtusha kuwa juu mwaka jana.

Shirika hilo la Umoja wa Mataifa limetahadharisha kwamba ulimwengu kwa sasa hauko katika njia sahihi ya kulifikia lengo la kupunguza visa vya malaria kwa asilimia 90 ifikiapo mwaka 2030.

WHO linasisitiza kwamba ufadhili unastahili kuongezwa mara ya mbili ya ahadi zilizokuwa awali.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents