Michezo

Gareth Southgate awatetea wachezaji wa Man United Chris Smalling na Luke Shaw

Gareth Southgate amabye ni kocha wa muda wa timu ya Uingereza amewatetea wachezaji wa Manchester United Chris Smalling na Luke Shaw, baada ya wao kulaumiwa na Meneja Jose Maurinho.

promo302789993

Mourinho aliwalaumu wachezaji hao kwa kukosa mechi ya Jamapili ambapo United walishinda Swansea mabao 3-1 akisema kuwa wangefanya vyovyote vile kuichezea timu hiyo.

mourinho_0310getty_875

Smalling ana jeraha la mguu naye Shaw alicheza mechi ya Alhamis ambapo Manchester United ilishindwa na klabu ya Fenerbahce.
Sasa Southgate anasema kuwa huenda kuna tatizo linalowakumba wachezaji hao wawili.

Smalling ambaye ana umri wa miaka 26 na Shaw 21, wameachwa nje ya kikosi cha Uingereza ambacho kitashiriki mechi ya kufuzu kwa kombe la dunia mwaka 2018 dhidi ya Scotland na mechi ya kirafiki ya wiki ijayo dhidi ya Uhispania.
Shaw amecheza mechi sita za ligi msimu huu tangu apone jeraha la mguu mwezi Septemba.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents