Burudani

Hii ndio sababu ya Halle Berry kuachana na mume wake Olivier Martinez

Halle Berry na Olivier Martinez wameachana kwasababu mume wake alihisi kuzidiwa mno kiuchumi na mke wake, imefahamika.

olivier-martinez-01-800

Wawili hao walikutana wakati wa kuigiza filamu, Dark Tide mwaka 2010 na muda mfupi wakawa miongoni mwa wapenzi wanaovutia Hollywood.

Halle alikuwa miongoni mwa waigizaji wa kike wakubwa na mumewe akiwa muigizaji maarufu Ufaransa aliyeanza kupata jina Marekani.

Lakini wiki hii walitangaza kuachana baada ya kudumu kwenye ndoa kwa miaka miwili na sasa mtandao wa People umedai kuwa masuala ya kazi na uchumi ndio yamekuwa chanzo.

Vyanzo vimedai kuwa mafanikio ya Halle yalimnyong’onyeza mume wake aliyeanza kuhisi dhaifu kwake.

Wakati wa ndoa yao, Berry alikuwa busy akifanya kazi za filamu na TV, wakati mume wake alikuwa akihangaika kupata nafasi Hollywood.

Katika kipindi cha ndoa yao, Berry, 49, aliigiza jumla ya filamu sita na series za TV, wakati Martinez, 49, alitokea kama mgeni tu kwenye vipindi vinne vya TV.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents