Uncategorized

Hivi ndivyo watu wenye ushawishi maarufu kama ‘Godfather’ wananvyoamua matokeo ya uchaguzi Nigeria

Watu wenye ushawishi mkubwa katika siasa za Nigeria mara nyingi hawagombei kiti chochote lakini watu wengi nchini humo wanaamini wao ndio huamua wakaoshinda au kushindwa.

Godswill Akpabio

Huku kampeini ya uchaguzi mkuu wa Februari 16 zikipamba moto kuna wanaume wenye ushawishi mkubwa wanaofanya kazi nyuma ya pazia.

Kwa mujibu wa Shirika la habari la BBC, wao ni wafadhili wa kisiasa ambao wanatumia pesa na ushawishi wao kupata uungwaji mkono wa wagombea wao.

Inaaminiwa kuwa wanasiasa ”hao”hawateuliwi kutokana na ukwasi wao wa kisiasa bali ni uwezo wao wa kulipa gharama ya wafadhili wao na kuwatajirisha zaidi.

Mpango huo umewafanya kubatizwa jina la “godfather”, anasema Dr Dele Ashiru, mhadhiri mkuu wa kitengo cha sayansi ya siasa katika chuo kikuu cha Lagos.

Gari lenye picha za wagombea wa APC katika jimbo la Akwa Ibom, Nigeria

“Jina hilo linatumika kuashiria mtu mwenye ushawishi mkubwa wa kisiasa ambaye anamteua mwanasiasa kijana ambaye anamuasili kama mgombea katika uchaguzi.

“Atafanya kila juhudi kuhakikisha mwanasiasa wake anateuliwa katika wadhifa wa kisiasa.

”Lazima wawe na ushawishi, wengi wao wana ushawishi huo kutokana na utajiri waliyo nao, au waliwahi kushikilia wadhifa wa kisiasa.”

Katika jimbo la kusini la Akwa Ibom, ambalo linazalisha mafuta kwa wingi, watu wengi wanaamini Godswill Akpabio, ambaye anashikilia kiti cha seneti ndiye mwenye ushawishi mkubwa.

Akpabio ambaye aliwahi kuwa gavana wa zamani wa jimbo hilo ana ushawishi mkubwa katika siasa za eneo hilo.

Ushawishi wake ni mkubwa wa kiasi cha kuwa hatua yake ya kuhamia chama tawala cha All Progressives Congress (APC) miezi kadhaa iliyopita imeipatia matumaini chama hicho kushinda kwa mara ya kwanza katika jimbo hilo tangu demokrasia ilipoimarika Nigeria mwaka 1999.

Wafuasi wa gavana anayeondoka wa jimbo la Akwa Ibom,Udom Emmauel wakiwa wamevalia kofia za kitamaduni

Hatua ambayo ilimfanya rais Muhammadu Buhari kuchagua jimbo la Akwa Ibom kuzindua kampeini yake mwezi Disemba mwaka jana.

Bw. Akpabio ameonesha uwezo wa kuwaleta wapya katika chama hicho. Hivi karibuni mmoja wa wafuasi wake amesema atawahamisha wapiga kura 300,000 kujiunga na APC.

Lakini seneta Akpabio amepinga kuwa na ushawishi kiasi hicho: “Nampinga mtu yeyote anaesema kuwa mimi ni ”godfather”.

“Wakati mbao naamini nilishikilia wadhifa huo ni mwaka 2015.

Nilimteua gavana wa sasa [wa Akwa Ibom] na nilipomtambulisha kwa watu walimuunga mkono,” aliiambia BBC.

Hata hivyo wanachama wa chama chake wanasema uchaguzi wa mwaka 2015 ulikumbwa na vurugu zilizopangwa na Bw. Akpabio.

Mkutano ya kisiasa ya chama APC katika jimbo la Akwa Ibom

Umana Okon Umana, aliyekuwa akiwania ugavana wakati huo, alimlaumu Bw. Akpabio kwa kutumia ushawishi wake serikalini ikiwa ni pamoja na vikosi vya usalama kumuidhinisha mgombea wake.

Aliielezea kama hali ambayo ”godfather” anakaa pembeni na mke wake “na kupanga orodha ya nani atakayeshiriki uchaguzi wa ugavana hadi nafasi za uwakilishi bungeni.

“Anaorodhesha majina haya kabla ya hata uteuzi kufanywa. Ikiwa jina lako halipo katika orodha hiyo wanahakikisha hupati nafasi ya kujumuishwa kwenye mchakato[wa uteuzi].”

Mwaka 2015 hata hivyo mahakama ya juu zaidi, iliamua kuwa uchaguzi ulikuwa huru na wa haki.W

Onofiok Luke, ambaye sasa ni spika wa bunge la jimbo la Akwa Ibom, alikuwa mwandani wa zamani wa kisiasa wa Bw. Akpabio.

Luke ambaye ni mfuasi mkubwa wa kidini, anaamini ufanisi wa ke wa kisiasa umetokana na baraka kutoka kwa mweyezimungu, lakini wengi wanasema amesaidiwa na na mwandani wake wa zamani wa kisiasa.

Godswill Akpabio amekanusha madai ya kuwahonga wandani wake wa zamani kisiasa

Aliwahi kuwa msaidizi wa kibinafsi wa Bw.Akpabio, na anakubali kuwa Bw. Apabio alifadhili harusi na hafla yake ya kusherehekea miaka 40 ya siku ya kuzaliwa na kwamba alichangia kuimarika kwake kisiasa

Uhusiano wao hata hivyo imeingia dosari baada juhudi za naibu gavana wa wa jimbo hilo kumshawishi spika huyo ambaye anadai alipewa dola milioni 5.5 (£4.2m) mwaka uliyopita ili kubadilisha chama kugonga mwamba.

“Nimefanya kazi nae nafahamu jinsi anavyoweza kutumia raslimali ya serikali kufikia malengo yake.”

Katika taarifa ya maadishi kupitia kitengo chake cha habari, Bi. Akpabio amekanusha madai yaliyotolewa dhidi yake, ikisisitiza kuwa: “Tunafahamu kuwa hiki ni kipindi cha kampeini na madai ya kila aina huibuliwana wapinzani kwa maslahi ya kisiasa.”

Wafuasi wa Rabiu Kwankwaso huvalia kofia nyekundu

Katika maeneo tofauti ya nchi, hatima ya baadae ya siasa ya Jimbo la Kano lenye waumini wengi wa dini ya kiislam huenda pia ikaamuliwa na wababe wa kisiasa wenye ushawishi mkubwa.

Kano ni ya pili kwa idadi kubwa ya wapiga kura waliyosajiliwa nchini, hali ambayo imefanya ushindi wa jimbo hilo kuwa muhimu kwa vyama vikuu viwili.

Gavana wa zamani Rabiu Kwankwaso, ana wafuasi wengi, ambao wanamuunga mkono kutokana sera ya elimu ya msingi bila malipo iliyozinduliwa wakati wa utawala wake. Mgomea yeyote atakaepata baraka zake ana uwezo wa kupata kura nyingi

Ameamua kumuunga mkono mgombea Abba Kabiru Yusuf, mgombea wa chama tawala(PDP), baada ya kutofautiana na washirika wake wa zamani.

Map of Nigeria showing Akwa Ibom and Kano states

Wanasiasa wote waliyozungumza na BBC wamejitenga na jina la “godfather” kwasababu linahusishwa na mienendo ya ubinafsi na tabia isyokuwa ya demokrasia.

Huku vijana wanaokulia chini ya kivuli watu hao wenye ushawishi wakiendelea kupata ukakamavu, haijabainika ikiwa wababe wao wa kisiasa wataendelea kudhiti uwezo wao madarakani

Kwa Bw Akpabio na Bw. Kwankwaso, itachukua muda mrefu kwa wao kugundua hilo.


Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents