Michezo

Hizi hapa mechi za kesho kuanza kwa mzunguko wa pili VPL

Ligi kuu soka Tanzania Bara inatarajia kuendelea tena hapo kesho kwa mzunguko wa pili kupigwa katika viwanja mbali mbali.

Singida United inayoshika nafasi ya nne katika msimamo wa ligi ikiwa na alama 27 nyuma ya mabingwa watetezi Yanga SC wenye pointi 28 inajipanga kuingia katika mzunguko wa pili hapo kesho siku ya Jumamosi kwa kuivaa Mwadui FC majira ya saa nane mchana katika uwanja wa Namfua.

Michezo mingine itakayo pigwa hapo kesho ni Azam FC waliyo nafasi ya pili kwa kujikusanyia alama 30 katika duru la kwanza itakuwa nyumbani dhidi ya Ndanda FC mechi itakayopigwa Azam Complex Chamazi jijini Dar es salaam.

Lipuli FC ya Iringa itakuwa na kibarua kizito nyumbani kwake itakapocheza dhidi ya Yanga SC iliyo maliza mzunguko wa kwanza kwa kuwa na pointi 28 ikiwa nafasi ya tatu mtanange utakaopigwa dimba la Samora, wakati Stand United ikiivaa Mtibwa Sugar uwanja wa CCM Kambarage Shinyanga.

Tanzania Prisons iliyo na alama 21 ikiwa nafasi ya 6 katika msimamo wa ligi wata wakaribisha Njombe Mji katika uwanja wa Sokoine Mbeya huku mchezo wa mwisho siku ya hapo kesho ni Majimaji FC itakapocheza na Mbeya City uwanja wa Majimaji Ruvuma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents