Habari

Huu ni uharamia mpya – Mwinyi

WAKATI Mkurugenzi wa Hali Halisi Publishers, Saed Kubenea, akiwasili India jana na kuanza matibabu, Rais mstaafu wa Awamu ya Pili, Alhaj Ali Hassan Mwinyi, amelifananisha shambulio dhidi ya waandishi wa habari na uharamia mpya.

na Eugenia Kimolo na Happiness Katabazi

 

WAKATI Mkurugenzi wa Hali Halisi Publishers, Saed Kubenea, akiwasili India jana na kuanza matibabu, Rais mstaafu wa Awamu ya Pili, Alhaj Ali Hassan Mwinyi, amelifananisha shambulio dhidi ya waandishi wa habari na uharamia mpya.

 

Akizungumza jana na waandishi wa habari nyumbani kwake Mikocheni, Dar es Salaam, Mwinyi alisema tangu kutokea kwa tukio hilo Jumamosi amekuwa akikosa usingizi.

 

“Kitendo hicho ni cha kutaka kuwanyamazisha waandishi ili msiandike maovu yanayotendeka, lakini nawaomba waandishi msikate tamaa na wala msitishike, fanyeni kazi bila kuogopa,” alisema Mwinyi.

 

Alitoa pole kwa wanahabari hao – Kubenea na Ndimara Tegambwage – waliovamiwa na kushambuliwa na watu wasiofahamika.

 

Katika shambulio hilo, Kubenea alimwagiwa kitu kinachoaminika kuwa ni kemikali yenye sumu na Tegambwage akakatwa mapanga.

 

Wakati huo huo, Kubenea amewasili salama nchini India. Na kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa watu walio karibu naye, aliwasili nchini humo jana asubuhi na kupelekwa moja kwa moja katika Hospitali ya Apollo iliyopo New Delhi.

 

Alipofika New Delhi alipokewa na ofisa mmoja kutoka ubalozi wa Tanzania nchini humo. Ofisa huyo alimpeleka katika ofisi za ubalozi ambako taratibu za kumfikisha hospitalini zilifanyika.

 

Wakati huo huo, katika mlolongo wa salamu za kulaani tukio hilo, Taasisi ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano ya Umma ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (IJMC) ilisema kuwa tukio hilo ni sawa na nia mbaya ya baadhi ya watu au kikundi cha watu waovu kupinga kwa makusudi juhudi za wanahabari katika kufichua maovu ndani ya serikali na jamii kwa ujumla.

 

Source: Tanzania Daima

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents