Burudani

Jibu la Casto iwapo Tunda naye atachora tattoo

Mara baada ya kuchora tattoo ya mpenzi wake Tunda, Mtangazaji wa kipindi cha Siz Kitaa kinachoruka Clouds TV, Casto Dickson amefunguka iwapo Tunda naye atafanya hivyo.

Casto amesema hadi kufikia hatua hiyo kuna jambo la tofauti baina yao na iwapo Tunda atafanya hivyo watu wataona.

“Utamuona akichora, kama akichora utamuona akichora, ana maamuzi yake, yeah!. Kwa sababu kuchora tattoo si pete sisi tumeanza hivi tuna sababu zetu,” amesema.

“Tuna maana yetu ambayo itakuja kuwa tofauti kabisa, for the first time in Africa tuseme, mtakuja kuona, yeah!,” Casto ameiambia Bongo5.

Mtangazaji huyo ameongeza kuwa hataki kuliweka suala hilo kuwa siku wakiachana atafuta hiyo tattoo na kueleza kwa upande wake hamna kitu kama hicho. Casto Dickson na Tunda mapenzi yao yalianza kugonga vichwa habari March 2018 pale walipoyaweka wazi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents