Burudani

Jux: Sikujua kama Jackie alikuwa akiuza unga

Inaonekana kuwa Jux hawezi kuyakwepa maswali kuhusu Jackie Cliff.

jackjack4

Uhusiano wao ulipata doa baada ya Jackie kukamatwa na madawa ya kulevya Hong Kong ambako hadi leo anatumikia kifungo. Lakini kwa mujibu wa muimbaji huyo wa ‘I’m Looking For You’, habari za kuwa mpenzi wake alikuwa akijihusisha na uuzaji wa madawa ya kulevya hadi kukamatwa, ilikuwa ngeni kwake kama watu wengine wote.

“Kiukweli nilimpenda sana Jackie Cliff maana mara nyingi mimi napokuwa na mtu huwa napenda kweli sababu huwa nahitaji kutulia,” alisema Jux kwenye kipindi cha Mkasi.

“Lakini huwezi amini sikuwahi kutambua kama Jackie Cliff anafanya mambo hayo mpaka alipopata matatizo hayo ndiyo najua mimi, hivyo ilinipa wakati mgumu sana mimi kiasi kwamba nilikuwa sijielewi,” aliongeza.

Hadi sasa haijulikani ni lini Jackie atamalizia kifungo chake.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents