Michezo

Kaka wa Pogba awapa presha United ‘Huitaji elimu ya chuo kikuu kufahamu Zidane anamuhitaji Pogba’

Kaka wa kiungo wa Manchester United, Paul Pogba ajulikanaye kwa jina la Mathias Pogba amesema kuwa wala huitaji elimu kubwa kufahamu Zinedine Zidane anavyomhitaji ndugu yake.

Paul Pogba was pushing for an exit in the summer but remains a Manchester United player

Mfaransa huyo, Paul Pogba alihusishwa na tetesi za kutimkia Real Madrid katika dirisha la usajili lililopita lakini mpaka sasa ameonekana kusalia Old Trafford.

Zidane hakuweza kufanikiwa kuweka mkwanja wa kutosha ili kuwashawi United kumuwachia nyota huyo licha ya kuonesha nia ya kuhitaji saini yake.

Mathias Pogba (right) says Zinedine Zidane's interest in his brother is no secret

Mathias Pogba ambaye anaitumikia klabu ya Manchego ya Hispania ameiyambia Radio Marca kuwa Zidane kuna wachezaji ambao aliwataka lakini hakuwapata.

”Zidane kuna baadhi ya wachezaji ambao aliwataka lakini hakuwapata, lakini sinashaka kwamba sasa anakwenda kufanya kazi ambayo alihitaji kuifanya ili kukirudisha kikosi katika ubora anao uhitaji.” Amesema Mathias Pogba.

”Mathias Pogba amesema ”Namkubali Zidane, anampenda kaka yangu kila mtu anafahamu hilo,” amemalizia Mathias Pogba.

Zinedine Zidane may yet revisit a move for Pogba in January or next summer

Juventus nayo ilihusishwa na dili la kumsajili Pogba katika dirisha la usajili lililopta lakini United ilishikilia dau la pauni milioni 150 ambalo ilihitaji.

Upande wa wakala wake, Mino Raiola ameendelea kusisitiza kuwa ” Kila mmoja anafahamu Pogba anahitaji kuondoka, kila mmoja anafahamu vile anavyojiskia Paul Pogba.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents