Burudani

Kala Jeremiah kufunga mwaka kwa kuachia audio na video ya ‘Walewale’

Rapper na balozi wa Pepsi, Kala Jeremiah anatarajia kufunga mwaka kwa kuachia wimbo mpya uitwao ‘Walewale’ sambamba na video yake. Kwenye wimbo huo, Kala amemshirikisha Neylee.

IMG-20131111-WA0000

Akizungumza na Bongo5 leo, Kala amesema angekuwa hajawatendea haki mashabiki wa muziki wake kama asingeachia wimbo mpya.

“Nikiwa kama msanii bora wa Hip Hop nimeona kuna umuhimu wa kufunga mwaka kwa Audio na Video ya wimbo wangu mpya ‘Walewale’ wimbo ambao utakuwa unaelezea maisha ya Watanzania kila siku. Nimemshirikisha mwanadada Neylee kwasababu ana sauti ya aina yake ndio maana nikaona nikifanya naye wimbo utatoka poa sana kutokana na aina ya uimbaji na sauti yake,” amesema Kala.

Wimbo huo unatarajia kutoka November 20.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents