Michezo

Kama mfungaji bora kweli, achukue kiatu cha dhahabu mara mbili mfululizo kama mimi – Harry Kane

Straika wa klabu ya Tottenham Hotspur, Harry Kane amempa changamoto mshambuliaji wa Liverpool, Mohamed Salah kuwa kama kweli anataka kutambulika kama mfungaji bora wa ligi kuu nchini Uingereza basi avunje rekodi aliyoiweka yeye ya kutwaa tuzo hiyo mara mbili mfululizo.

Mshambuliaji wa timu ya Liverpool, Mohamed Salah

Salah amefunga jumla ya mabao 32 ligi kuu ya Uingereza msimu huu huku akifunga wakati Liverpool ikiibuka na ushindi wa mabao 4 – 0 dhidi ya Brighton hapo jana siku ya Jumapili na kufanikiwa kutwaa kiatu cha dhahabu akimzidi mpizani wake ambaye ni straika wa Tottenham, Kane kwa mabao mawili baada ya kumaliza ligi kwakufunga 30.

Straika wa klabu ya Tottenham Hotspur, Harry Kane

Kupitia mahojiano yake na vyombo vya habari Kane amesema nivizuri kuwa na ushindani na inavutia kuona kwenye ligi ya Uingereza kunakuwa na wachezaji wawili waliyofanikiwa kufunga mabao 30.

Nivizuri kuwa na ushindani, na inavutia zaidi kuona kwenye ligi ya Uingereza kunakuwa na wachezaji wawili waliyofanikiwa kufunga mabao 30.

Binafsi yalikuwa ni malengo yangu kuona kipaji changu kinakuwa ukilinganisha na mwaka jana, wakati nilifunga mabao 29 msimu huu nimefikisha 30 kwangu naona vizuri.

Mo amefanya vizuri mwaka huu, hakika anastahili kupata tuzo hiyo ya kiatu cha dhahabu naangazia zaidi kwenye ushindani wetu mwaka ujao.

Kila mchezaji anahitaji kuwa na muendelezo mzuri kila msimu na hiyo ndiyo tafsiri ya mchezaji mzuri kuwa bora. Amefanya kitu kizuri na kinashangaza msimu huu na anaonekana kuwa mchezajibora tutaona kama tutaendelea kuwa hivi msimu ujao.

Licha ya kupoteza tuzo hiyo, Kane mwenye mabao 30, anaamini kuwa amefanya vema zaidi msimu huu baada ya misimu miwili iliyopita kufunga 25 na 29 na kuongoza kuchukua kiatu cha dhahabu mara mbili mfululizo.

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents