Burudani

Katika muziki ushirikina upo – Man Fongo

Msanii wa muziki wa Singeli, Man Fongo amefunguka tetesi za kufanyiwa ushirikina katika muziki wake ili asifanye vizuri.

Muimbaji huyo ameiambia Times Fm kuwa hawezi kujua hilo moja kwa moja kwa sababu yeye ndiye msanii mkubwa kuliko wote katika muziki huo ila ushirikina ni kitu ambacho kipo katika muziki.

“Katika muziki mambo ya ushirikina yapo lakini huwezi ukamshawishi mtu ukasema mtu fulani hamna ila vitu vinatokea, hivyo ushirikina upo,” amesema.

Ameongeza kuwa licha ya hayo yote hakuna anayeweza kushusha nyota yake kimuziki kwa sasa. Man Fongo kwa sasa anafanya vizuri na ngoma yake mpya ‘La Nafasi’.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents