Michezo

Kenya yamtambulisha Mfaransa, Sebastien Migne  kuwa kocha wa Harambee Stars

Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini Kenya limemtangza Mfaransa, Sebastien Migne kuwa kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Harambee Stars kwa muda wa miaka mitatu.

Migne  mwenye umri wa miaka 45, amerithi mikoba ya Paul Put aliyeamua kuachiangazi katikati ya Mwezi Februari.

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini Kenya, Nick Mwendwa  amesema kuwa lengo lao kubwa ni kufanikiwa kushiriki michuano ya kombe la dunia ijayo.

Hata hivyo, Mwendwa wamemuahidi kocha huyo kumpatia ushirikiano wa hali ya juu huku akisema kuwa wamezungumza na Serikali katika kuhakikisha wanatoa ushirikiano wake kwa Sebastien Migne.

Kwa épande wa Sebastien Migne amesema kuwa anajisikia furaha kuwepo Kenya huku akiamini kuwa atakutana na changamoto mpya.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents