Michezo

Kila atakayebahatika kuifunga goli Tanzania kuzawadiwa laki 5 na Rais wa ZFF, ni mechi ya kufa na kupona (+Video)

Mwenyekiti wa kamati ya soka kwa vijana  Zanzibar, Seif Baus amesema kuwa Rais wa shirikisho la soka visiwani humo Seif Kondo Pando  amewaahidi wachezaji wa timu ya U20 kuwapatia kiasi cha laki tano kwa kila mchezaji atakefunga bao kwenye mchezo muhimu wa leo utakao pigwa hapo baade majira ya saa 10 dhidi ya ndugu zai wa Watanzania Serengeti Boys kwenye michuano ya CECAFAU20 inayoendelea nchini Uganda.

Timu ya Taifa ya Zanzibar ya Vijana U-20 (Karume Boys) imefudhu hatua ya robo fainali kwenye Mashindano ya Cecafa Chalenj Cup yanayoendelea Uganda baada ya Ethiopia kufungwa mabao 4-0 na Kenya mchezo wa kundi B uliochezwa saa 7 mchana kwenye uwanja wa Njeru nchini Uganda.

Hivyo Zanzibar kuungana na Kenya na Tanzania bara katika hatua ya robo fainali kutoka kundi hilo B Na aajira ya Saa 10:00 jioni leo utachezwa mchezo wa mwisho wa kundi hilo kati ya Zanzibar dhidi ya ndugu zao Tanzania bara ambapo timu zote zimeshafudhu wanagombea kumaliza nafasi ya pili.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents