MichezoUncategorized

Tuzo ya Messi utata mtupu, baadhi ya makocha wadai hawakumpigia lakini kura zao zakutwa kwake, FIFA yatakiwa kutoa maelezo

Kumekuwa na utata juu ya shirikisho la soka duniani FIFA kumpa baadhi ya kura za uchezaji bora nyota wa klabu ya Barcelona na timu ya taifa ya Argentina, Lionel Messi ambazo hakustahili kwa mujibu ya waliopiga.

Usiku huo ulishuhudiwa Muargentina, Messi akimzidi kwa kura beki wa Liverpool, Virgil van Dijk na mshindi mara tano, Cristiano Ronaldo na kutangazwa kuwa mchezaji bora wa FIFA mwaka 2019.

Utata huo umeibuka baada ya hapo jana siku ya Jumatano Shirikisho la soka la nchini Misri (EFA), Kocha Mkuu wa timu ya taifa ya Sudan na Nahodha wa timu ya taifa ya Nicaragua, Juan Barrera kilammoja akidai kuwa hawakumpigia Messi lakini cha kustaajabisha kura zao zimeonekana kwa Muargentina huyo.

Shirikisho la soka la nchini Misri (EFA), hapo jana siku ya Jumanne imeitaka FIFA kutoa maelezo ya kwanini kura za kocha wao wa timu ya taifa na nahodha wake walizo mpigia mchezaji Mo Salah hazikuhisabiwa.

Kocha Shawki Ghareeb na nahodha, Ahmed El-Mohammadi kura zao hazikutajwa na shirikisho la mpira wa miguu duniani FIFA katika usiku wa huo wa tuzo Jumatatu.

Related image

“Shirikisho la soka nchini Misri lilituma kura yake FIFA 15 Agosti, siku nne kabla ya tarehe rasmi ya kutuma kufungwa,” limesema Shirikisho la soka la nchini Misri (EFA).

”’Tumeiuliza FIFA kwanini kura ya Misri haijakukubalika, tunafungua uchunguzi wa wazi juu ya hili,” iliongeza taarifa hiyo ya shirikisho la soka la Misri.

Siku ya Jumatano kocha wa timu ya taifa ya Sudan, Zdravko Lugarisic na Nahodha wa timu ya taifa ya Nicaragua, Juan Barrera kupitia mitandao ya kijamii wamesema kuwa kura zao zilizotangazwa na FIFA haziendani na waliempigia.

Lugarisic amesema kura yake alimpigia mchezaji wa timu ya taifa ya Misri, Mohamed Salah lakini FIFA imeonyesha amempigia Messi.

Kwa upande wake,Barrera amesisitiza kuwa hakumpigia kura Messi na kulilaumu shirikisho la soka duniani FIFA.

Image result for messi best player vs egypt and sudan coach

‘‘Sikumpigia kura Messi. Nimeshangaa kuona kura yangu imewekwa katika orodha ya watu waliyompigia Messi na wala hakuna maelezo ya kwanini imewekwa pale.” amelalamika Barrera.

Hata hivyo kupitia akaunti ya Twitter ali ‘screenshot’ kura aliyopiga na kuweika ili watu waweze kuona aliyempigia.

 

Shirikisho la Misri linatumaini nyota wake Mo Salah atakuwa mwenye amani sasa baada ya kuona hakupigiwa kura na taifa lake na kuonyesha hasira kwa kufuta baadhi ya vitu ambavyo vinaonesha utaifa wake kupitia kwenye akaunti yake ya Twitter.

https://twitter.com/ahmz_osman/status/1176486392068825089?s=20

Kura pekee ya Mo Salah aliyoone ni le aliyopigiwa na mwandishi wa habari, Hany Danial na kuandika hisia zake juu ya tukio hilo la kutokuona kura alizopigiwa kutoka Misri.

“Haijalishi ni kwa kiasi gani watajaribu kubadilisha upendo wangu kwenu na watu wenu, kamwe hawataweza kufanya hivyo,” ujumbe ambao ulikuwa unalenga taifa lake.

Cameroon legend, Samuel Eto’o ambaye aliudhuria usiku huo wa tuzo aliwaambia waandishi wa habari kuwa wachezaji bora kwa upande wake ni Salah na Mane.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents