MichezoUncategorized

Klabu za Newcastle na West Ham zilivyovamiwa na maofisa wa mamlaka ya mapato na forodha

Makao makuu ya klabu ya Newcastle United pamoja na ile ya West Ham yalivamiwa mapema jana na maofisa wa Mamlaka ya Mapato na Forodha ya nchini Uingereza, ikiwa ni sehemu ya uchunguzi wa kodi.

Maafisa hao wa mapato na Forodha waliotumika katika uvamizi wa ofisi hizo za klabu, waliweza kuingia mpaka ndani ya dimba la mazoezi ya klabu hizo na kisha kuingia katika ofisi kuu za klabu ya Newcastle United St James’ nyakati za saa 6:30 kwa masaa ya nchini Uingereza. Baadaye walimalizia katika Dimba la London ambako ndio nyumbani kwa klabu ya West Ham.

Idadi ya waliokamatwa imetokana na kiasi cha Dola Milioni 5 iliyotuhumiwa kua ni ya kodi ya mapato pamoja na makaridio ya Bima ya Taifa ambayo imeonekana kufanyika kwa Udanganyifu. Chombo cha Habari za Michezo cha Sky sport, kinaamini kuwa moja ya wahusika katika sakata hilo ni Mkurugenzi wa Newcastle Lee Charnley.

Taarifa kutoka “HMRC inaeleza kuwa wamekamatwa watu kadhaa pamoja na wafanyakazi katika sekta ya mpira wa miguu ambao wametuhumiwa kuhusika na ubadhilifu huo wa mapato ya kodi pamoja na Bima ya Taifa.

Zaidi ya Maofisa “180 wa Mamlaka ya Mapato na Forodha ya nchini Uingereza wameanza uchunguzi Kaskazini Mashiriki na Kusini Mashariki mwa Uingereza na kuzidi kuwakamata watu pamoja na kupitia kumbukumbu za Biashara, kumbukumbu za Fedha, Kompyuta pamoja na simu Mkononi.

BY HAMZA FUMO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents