Michezo

Kujiuzulu Mwenyekiti wa Simba bado kitendawili, kamati ya uchaguzi yadai haijapata barua rasmi ya Mkwabi

Makamu Mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi wa klabu ya Simba, Steven Ally amesema kuwa mpaka sasa haijapata barua rasmi ya kujiuzulu kwa Mwenyekiti wa timu hiyo, Swedi Mkwabi bali inaona taarifa hizo kupitia kwenye mitandao ya kijamii tu.

Image

Steven ambaye alikuwa miongoni mwa wajumbe watano waliyo teuliwa katika Kamati ya Uchaguzi ambayo ilitangazwa Agosti 2018 na kuwezesha kupatikana kwa Mwenyekiti, Swedi Mkwabi yeye akiwa Makamu Mwenyekiti, amesema hawana taarifa ya maandishi ya kujiuzulu kwa kiongozi huyo.

Makamu huyo mwenyekiti, Steven Ally ameyasema hayo hii leo kupitia mahojiano yake na chombo cha habari cha EFM Radio kupitia kipindi chao cha michezo.

Steven Ally amesema Kama itatokea habari za kujiuzulu kwa Swedi Mkwabi ni za kweli kama wao wanavyoona kupitia kwenye mitandao ya kijamii basi maana yake nafasi ya Mwenyekiti itakuwa ipo wazi na hivyo wajumbe waliyochaguliwa watalazimik kumteuwa mmoja mwenye sifa ili kuweza kukaimu kwa muda.

”Kama itatokea manayake nafasi ya Mwenyekiti itakuwa ipo wazi, ili mambo yaende na ya sisimame itabidi wajumbe ambao walichaguliwa watamteuwa mmoja ili akaimu ambaye anasifa za kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti.”- Amesema Steven Ally Makamu Mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi wa klabu ya Simba.

Steven Ally ameongeza ”Miongoni mwa wale wajumbe waliyopo aliyetimiza hizo sifa kama za Mkwabi achukue hiyo nafasi kwa muda akikaimu huku maandalizi ya uchaguzi yanafanyika lakini kama ni kweli Mkwabi amejiuzulu maana mimi nimeona kwenye mitandao ya kijamii tu na hakuna barua rasmi.”

Kutokuwepo kwa Mkwabi kunaiyathiri vipi Simba SC hasa katika upande wa wanachama kutokana na yeye kuwa mwakilisha ndani ya bodi ambayo pia inaunganisha mdhamini mkuu.

”Swala la kutumikia wananchi ama watu waliyokuchagua ni swala la kikatiba, Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inampa mtu uhuru wa kuchagua na kuchaguliwa, lakini pia inatoa uhuru wa mtu pale atakapoona hiyo kazi anashindwa kuimudu kwa sababu moja ama nyingine basi aiyachie.”

”Ingekuwa kosa zaidi kama angebaki ilihali kazi zake zinambana kufanya majukumu ya klabu, kwahiyo mimi naona sidhani kama hajawatendea haki wanachama bali amewatendea haki kwa kuwachia nafasi hiyo kwakuwa anamambo mengine yanamkaba.”

Swali la kujiuliza je hayo mambo mengine hakuwa nayo wakati anawania nafasi ya Mwenyekiti ndani ya Simba SC ?,

”Mimi siwezi kumsemea lakini ni kwamba hii nafasi ya Mwenyekiti ya mfumo mpya wa Simba SC yeye ni wakwanza kwahiyo kila mtu alivyoingia alikuwa na mtazamo wake kwamba kazi itakuwa hivi na hivi na labda ameona ni tofauti, nisingependa kumsemea lakini mimi naelewa katika haya mambo unaweza kujiuzulu ni haki yako na kama sababu ndiyo kama zile zilizoelezwa kwenye mitandao ya kijamii ndiyo zenyewe ni jambo la msingi. Sijawahi kusikia ndani ya Simba kunatatizo.”

https://www.instagram.com/p/B2YovezH3Jz/

Taarifa za kujiuzulu kwa Mwenyekiti wa Simba zilienea juma lililopita huku kwa upande wa klabu hiyo hukiandika ujumbe huu.

”Uongozi wa klabu ya Simba unatoa taarifa kwa wanachama, mashabiki na wananchi wote kwamba Mwenyekiti wa Klabu ya Simba, Swedi Mkwabi kwa uamuzi wake mwenyewe amejiuzulu nafasi ya Uenyekiti.” Iliandika Simba SC kupitia akaunti yake ya Instagram.

Simba iliongeza ”Katika barua ambayo Swedi ameiandikia Bodi ya Wakurugenzi kupitia Mwenyekiti wa Bodi amesema sababu kuu ya kijiuzulu nafasi hiyo ni kuhitaji muda zaidi kusimamia shughuli zake binafsi.”

”Bodi ya Wakurugenzi na Sekretarieti ya Simba inamtakia kila la heri katika shughuli zake, na tunatumaini kwamba ataendelea kushiriki katika shughuli mbalimbali za klabu kama ilivyokuwa awali kabla kupata nafasi hiyo. Utaratibu wa kumpata Mwenyekiti mpya tutawatangazia hapo baadae.”

Kabla na hilo mara kadhaa kulikuwa na taarifa zisizo rasmi kuwa ndani ya klabu hiyo mambo sio shwari, hasa kwa upande wa wanachama wenye hisa 51 na ule wa mwekezaji mwenye hisa 49. Ikidaiwa mwekezaji kuwa na nguvu zaidi ya wale wenye hisa 51.

Wakati sababu zinazodaiwa kupelekea kujiuzulu kwa Mwenyekiti wa Smiba SC, Swedi Mkwabi ni kwamba anataka kufanya shughuli binafsi na majukumu yamekuwa ni mengi zaidi.

Lakini swali la kujiuliza ni kwamba  kabla ya kuwa Mwenyekiti ndani ya klabu hiyo shughuli zake binafsi alikuwa nazo, je hiyo inawezekana kuwa sababu ya msingi ya yeye kuwachia ngazi ?.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents