Uncategorized

Kundi la Weusi Kutoa Album yao ya Kwanza


Kundi la muziki wa Kizazi kipya toka A-Town (Arusha), Weusi Entertainment, linatarajia kuachia albamu yao wiki ijayo iitwayo ‘Muziki Mzuri’.
Msemaji wa kundi hilo, Nick Simon amesema album hiyo itakuwa na nyimbo 20, ambapo imehusisha nyimbo za wasanii Joh Makini, Lord Eyes, Bonta, Nick na Gnako.

“Albamu ipo katika hatua za mwisho kukamilika na tumeifanya katika studio tofauti ili kuleta mchanganyiko wa ladha. Tunakusudia kuisambaza wenyewe kupitia mawakala wetu waliopo Dar es Salaam, Arusha, Mwanza na mikoa mingine ili kuepukana na ulanguzi uliopo sasa hivi,” alisema.

Wasanii walioshirikishwa katika albamu hiyo ni Juma Nature, Peter Msechu, Belle 9, Pipi na Fundi Samweli

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents