Burudani

Kwanini ‘Nashindwa’ haichezwi MTV Base, Trace? Christian Bella aitaja sababu

Nashindwa ya Christian Bella ni miongoni mwa video nzuri za nyimbo zilizoongozwa na Adam Juma lakini hazijawahi kuchezwa kwenye vituo vya runinga vya kimataifa.

IMG_0371

Akizungunza na 255 ya XXL kupitia kituo cha redio cha Clouds FM, Bella alisema baada ya kuituma kwenye vituo hivyo aliambiwa video hiyo ina vitu vya kurekebishwa ili iweze kuchezwa. Kwa lugha nyingine haikukidhi viwango wanavyohitaji.

“Adam alichosema kuna vitu amebadilisha lakini mimi sikwenda kuichukua, lakini mimi niliachana nayo tu sijui kwanini. Nilijua kuna kitu kingine kinakuja,” alisema.

“Mimi nikishatoa ngoma naona basi hii ishakwisha natafuta nyingine. Lakini nashukuru inapigwa kwenye television za Congo sasa hivi. Kwahiyo imeenda mpaka kule. ‘Nani Kama Mama’ na ‘Nashindwa’ zinapigwa kwenye channel kubwa za kule halafu Kinshasa kuna ugumu wa game lakini zinapigwa. Wamegundua kuna mtu anafanya vizuri huku,” aliongeza Bella.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents