BurudaniVideos

Label mpya ya muziki ‘Instincts Records’ iliyopania kuleta mapinduzi Bongo yazinduliwa (Video)

Label mpya ya muziki iitwayo Instincts Records imezinduliwa rasmi Jumamosi hii jijini Dar es Salaam.

Kwenye uzinduzi huo uliofanyika Regency Park Hotel na kuhudhuriwa na mastaa mbalimbali, msanii wa kwanza wa label hiyo, Shose alitambulishwa rasmi pamoja na kuoneshwa video ya wimbo wa kwanza, ‘Falling in Love’ iliyoongozwa na Hanscana.

Mtangazaji wa Times FM, Moko Biashara akiwa host kwenye uzinduzi huo

CEO wa label hiyo, Joseph Mwanukuzi, ameiambia Bongo5 kwenye uzinduzi huo kuwa Instincts Records imekuja kuleta mapinduzi makubwa kwenye muziki wa Tanzania.

Amedai kuwa lengo la kuanzisha label hiyo ni kutokana na kuwepo kwa malalamiko ya wasanii wengi wenye vipaji ambao wamekosa msaada.

Mwanukuzi amesema msanii akiwa Instincts hupatiwa mambo yote muhimu anayohitaji ili kuishi na yeye kujikita katika kutengeneza muziki pekee. Ameongeza wamepanga kusaini wasanii wanne kila mwaka na tayari wapo kwenye mazungumzo na wasanii kadhaa na watachuja wa kuwasainisha kutokana na vigezo wanavyotaka.

“Ni kazi kidogo kuingia Instincts lakini pindi umeingia Instincts Records inabidi uilaumu Instincts usipotoka,” amesema Mwanukuzi.

Amesisitiza label yake ina malengo makubwa yakiwemo kuhakikisha kuwa msanii wao anatajwa kwenye tuzo kubwa kama Grammy au anatumbuiza kwenye tuzo za BET.

“Sijaona mimi msanii ambaye ameenda Marekani, wote wasanii wa Tanzania na namaanisha wote, ambaye ameenda ikatangazwa BET kwamba fulani yuko hapa ametoka Tanzania.Sasa nataka Instincts Records sisi tutoe. Hilo ndio lengo langu na namuomba Mungu anisaidie,” Mwanukuzi ambaye ameishi nchini Marekani kwa miaka kumi na saba ameeleza.

Kwa upande wake Shose ambaye ni msanii wa kwanza kusainishwa kwenye label hiyo, amedai kuwa ni bahati kwake kuwa chini ya usimamizi wa label ambayo imejipanga vizuri.

Shose ambaye amedai kuwa aliwahi kufanya kazi na Machozi Band kwa muda mfupi, amesema ana matarajio kuwa akiwa chini ya Instincts atafanya kazi nzuri na hatowaangusha Watanzania.

Producer Abbah naye atakuwa chini ya label hiyo na ndiye aliyetayarisha wimbo wa Shose, Falling In Love

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents